Pages

AAAAAAAAAAAA

AAAAAAAAAAAAA
Kanisa Anglikana Tanzania-Dayosisi ya Dar es Salaam, Mtaa wa Mtakatifu Mathayo-Majohe

Nyumba ya Padri wa Mtaa iliyopo eneo la kanisa iliyojengwa kwa matoleo ya waumini wakiongozwa na Padre Patrick Challo

Ofisi za kanisa na darasa la 'Sunday School'

Jumamosi, 17 Machi 2018

Muonekano wa mbele wa Gazeti Upendo la kesho


Picha 10 za makaburini msiba wa Domic Lucas Peter

Majane wa marehemu akiweka shada la maua kwenye kaburi

Ni vilio na majonzi vilitawala nyumbani kwa marehemu Dominic Peter aliyefariki jana alfajiri baada ya kuanguka ghafla nyumbani kwake Chuo Rada, Majohe-Dar es Salaam. Ibada iliongozwa na Padre Johson Lameck wa Kanisa Anglikana Mtakatifu Mathayo Majohe-Dar es Salaam, huku Padre Patrick Challo akitoa mahubiri mazuri na yenye funzo kubwa kwa waombolezaji. Pia walikuwepo Wainjilisti Sospeter Mrope na John Haule kwenye ibada hiyo. Baada ya ibada mazishi yalifanyika makaburi ya Kwanamtumbo Majohe-Dar es Salaam. Marehemu ameacha mjane na watoto watano. Bwana ametoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe. Amina 

Picha 14: Kilichojiri nyumbani kwenye msiba wa Dominic Lucas Peter

Ni vilio na majonzi vilitawala nyumbani kwa marehemu Dominic Peter aliyefariki jana alfajiri baada ya kuanguka ghafla nyumbani kwake Chuo Rada, Majohe-Dar es Salaam. Ibada iliongozwa na Padre Johson Lameck wa Kanisa Anglikana Mtakatifu Mathayo Majohe-Dar es Salaam, huku Padre Patrick Challo akitoa mahubiri mazuri na yenye funzo kubwa kwa waombolezaji. Pia walikuwepo Wainjilisti Sospeter Mrope na John Haule kwenye ibada hiyo. Baada ya ibada mazishi yalifanyika makaburi ya Kwanamtumbo Majohe-Dar es Salaam. Marehemu ameacha mjane na watoto watano. Bwana ametoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe. Amina
Jeneza likiwasili nyumbani
Meza ya watumishi walioongoza ibada: Toka kulia ni Mwinjilisti John Haule, Fr. Johnson Lameck, Fr. Patrick Challo na Mwinjilisti Sospeter Mrope
Katikati mwenye mavai meupe na kilemba cheupe ni Mjane (mke wa marehemu)
Fr. Challo akihubiri
Jeneza likiwa ndani mwa nyumba ya marehemu
Jeneza likiwa ndani mwa nyumba ya marehemu
Mjomba wa marehemu akisoma historia

Picha zifuatazo ni wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa marehemu. Ndugu wa karibu wakionekana kulia kwa uchungu huku wakisaidiwa


Ijumaa, 16 Machi 2018

TANZIA (Dominic Luka)

Dominic Luka ametwaliwa na Bwana usiku wa kuamkia leo baada ya kuanguka ghafla nyumbani kwake. Msiba upo nyumbani kwake Chuo Rada-Majohe-Dsm. Marehemu alikuwa Katibu msaidizi wa Jumuiya ya Mt. Petro, Kanisa Anglikana Mt. Mathiya-Viwege. Taarifa toka kwa Mwinjilisti Sospeter Mrope (0713355943). 

Bwana ametoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe. Amina.

Alhamisi, 15 Machi 2018

Pumzika kwa amani Padre Onesphory Kayombo


Pd. Onesphory Lazaro Kayombo (C.PP.S) (58) pichani juu amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Kinondoni Jijini Dar alikokuwa amelazwa. Padre Kayombo alikuwa akitumika kanisa Katoliki Parokia ya Tegeta-Dar es Salaam.

Padre Kayombo ni tunda la kwanza kabisa la Wamissionari wa Damu Azizi ya Yesu kutoka Manyoni, Singida. Shirika linapoadhimisha Jubilei ya miaka 50 ya uwepo na utume wake nchini Tanzania linamwangalia Padre Kayombo, maarufu kama Kalikenye kwa jicho la pekee. Na kutoka Manyoni, Shirika linaendelea kupata miito ya kimissionari, kielelezo cha ushuhuda wenye mvuto na mashiko! Katika maisha na utume wake, amekuwa ni Paroko na Jaalim Seminari kuu ya Peramiho, Jimbo kuu la Songea.

Tarehe 29/10/2016 alifanyiwa jubilee ya kutimiza miaka 25 ya Upadri katika Parokia ya Kupaa na Bwana, Manyoni-Singida.

Kwa taarifa zaidi kuhusu msiba huu tembelea ukurasa wa facebook wa Radio Maria https://web.facebook.com/radiomaria.tanzania/

Padre Kayombo akiwa na waumini wa Parokia ya Kupaa na Bwana, Manyoni-Singida siku ya kuadhimisha miaka 25 ya Upadri wake.

Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe. Amina

Jumanne, 13 Machi 2018

Mchungaji Tuheri apumzishwa kwenye nyumba yake ya milele

Hapa ndipo alipopumzishwa jana aliyekuwa Mchungaji wa KKKT-Magogoni-Kigamboni-Dsm, Mchungaji Tuheri Aaron. Ni Manerumango, Mkuranga, Pwani. Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.
Picha kwa hisani ya Upendo Media

Jumapili, 11 Machi 2018

Picha 6: Mchungaji Tuheri asafirishwa kwenda Manerumango kwa mazishi

Ilikuwa tarehe 8/3/2018 Bwana alipomtwaa mtumishi wake Mchungaji Tuheri Aaron wa Usharika wa Magogoni KKKT - Kigamboni. Kifo chake kilitokea usiku kwa ajali ya gari akitokea Mbagala, Dar es Salaam. Waumini na waombolezaji wengine wakiongozwa na Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dkt. Alex Malasusa walipata fursa ya kumuaga leo kwenye ibada iliyofanyika usharikani magogoni KKKT Kigamboni na baadae saa moja jioni kusafirishwa kuelekea Manerumango mkoani Pwani kwa mazishi. Marehemu ameacha mjane na watoto wawili. Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi. Amina
 
 Jeneza likitolewa nje baada ya ibada kanisa KKKT usharika wa Mgogoni-Kigamboni ambapo ibada ya kumuaga Mch. Tuheri ilifanyika leo
Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dkt. Alex Malasusa wa mwisho kulia, akitoka nje ya kanisa KKKT usharika wa Mgogoni-Kigamboni ambapo ibada ya kumuaga Mch. Tuheri ilifanyika leo


Mch. Tuheri enzi za uhai wake

Video: Maharusi wakiingia ukumbini, harusi ya Dismas & Agnes.

Maharusi Dismas na Agnes wakiingia ukumbini Cavilam Dodoma tarehe 8 Des 2017. Tazama video hapo chini.

Audio: Sikiliza mahubiri ya Padre Johnson ibada ya pili leo

Sikiliza mahubiri ya Padre Johnson Lameck ibada ya pili leo hapo chini.


Ratiba ya sikukuu za jumuiya 2018


Masomo na nyimbo za ibada za leo


Picha 2: Jumuiya ya Mt. Yohana yawategemeza watumishi

Leo wana jumuiya ya Mtakatifu Yohana  ya hapa mtaani wamewategemeza watumishi wa madhabahuni. Pichani juu ni baadhi ya vitu vilivyotolewa na Jumuiya hiyo. Mungu awabariki sana.
 Baadhi ya wanajumuiya ya Mtakatifu Yohana