Pages

AAAAAAAAAAAA

AAAAAAAAAAAAA
Jumapili, 21 Februari 2016

Matukio katika Semina ya kazi

Meza kuu, toka kushoto ni Fr. Patrick Challo ambaye ndiye aliyeongoza semina, akifuatiwa na Mwinjilisti John Haule na Mwinjiisti Sospeter Mrope toka kigango cha Viwege.

Semina ilianza saa 4:30 asubuhi na ilihusisha viongozi wote wa kanisa pamoja na wale wa Kigangoni (Viwege). Iliongozwa na Fr. Challo ambaye alifundisha mambo mengi sana kuhusu uongozi. Mwisho wa Semina wana semina walionekana kuridhishwa sana na mafundisho hayo ambayo yalizingatia mambo yafuatayo:-
  • Mungu anapotaka kukutumia lazima ajitambulishe kwako
  • Uhusiano wa kiongozi na Mungu. Yohana 15:1-15
  • Uhusiano wa kiongozi na familia yake. 1Timotheo 3:4-5
  • Uhusiano wa kiongozi na watu awaongozao.
  • Mpango mkakati wa ujenzi wa kanisa


 Wana semina wakipata chai maandazi kabla ya semina kuanza.
Baada ya kufungua semina kwa maombi Fr. Challo aliendelea na semina. Pichani anaonekana akifundisha huku wana semina wakimsikiliza kwa makini sana.
 Wana semina wakipumzika kwa dakika 10 kabla ya kuendelea na sehemu ya pili ya semina

Mhazini wa kanisa Bw. Semaganga akitoa mchango wake kwa wana semina. Pia Fr. Challo alimsifu sana Bw. Semaganga kwa utendaji wake.
 Mke wa Fr.Challo akirejea kwenye kiti chake baada ya kutoa neno fupi kwa wana semina
 Viongozi toka Kigango cha Viwege walioshiriki katika Semina
Semina ilikamilika kwa viongozi kupata chakula kitamu. Baada ya chakula wana semina walitawanyika.