Pages

AAAAAAAAAAAA

AAAAAAAAAAAAA
Jumapili, 13 Machi 2016

Mnada wa wana UKWATA toka Chuo Rada Majohe wafana

Mzee Njama ndiye aliyetuendeshea mnada. Pichani anaonekana ameshika nazi tayari kwa kuzinadi.

Leo tulisali na wana UKWATA toka Chuo Rada Majohe. Ujio wao uliambatana na mnada ili kuwawezesha kupata kipato cha kufanya Mahafali yao ambayo yatafanyika mwezi April mwaka huu. Mnada huo ulifanyika ibada ya kwanza na ya pili. Tunashukuru Mungu kwa kiasi kilichopatikana.
 Wakristo wakifuatilia kinachoendeleakwenye mnada
 Mzee Njama akiwa ameshika maembe na apple tayari kwa kuvinadi
Mzee Njama akitoka kumkabidhi Fr. Challo embe na apple baada ya kununuliwa na mkristo mmoja. Embe jingine alikabidhiwa Bibi Winie baada ya kugongana bei.
 Leso na Mwamvuli mdogo vikinadiwa
 Wana UKWATA wakifuatilia mnada wao kwa makini
 Mkristo akifurahi baada ya kufanikiwa kununua leso na mwamvuli katika mnada huo
 Mayai ndani ya mfuko yakinadiwa
Mpiga picha alifanikiwa kununua mayai, akajipiga picha mwenyewe