Pages

AAAAAAAAAAAA

AAAAAAAAAAAAA
Jumapili, 6 Machi 2016

Picha na Video za uzinduzi wa awali wa tovuti ya Kanisa

Ilikua ni furaha isiyo kifani kwa wakristo wa Kanisa Anglikana Mt.Mathayo Majohe Dar es Salaam baada ya kuona jina la tovuti yao likitokea kwenye 'projector screen' iliyokua mbele ya kanisa kuashiria uzinduzi wa tovuti hiyo leo. Jina la tovuti ni www.anglikanamajohe.com .Baada ya kuona jina hilo walipata fursa ya kuitazama tovuti kwa kupitia ukarasa mmoja mmoja.

Pia kanisa lina ukurasa wake wa facebook kupitia linki hii www.facebook.com/anglikanamajohe. Wote mnakaribishwa kuitembelea tovuti na ukurasa wa kanisa wa facebook ili mpate taarifa nyingi kuhusu kania.

Uzinduzi huu wa tovuti ni wa awali, uzinduzi mkubwa unatarajiwa kufanywa baadae na Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Valentino Mokiwa.

Wakristo wakifurahia uzinduzi huo, wengine wakipiga picha za kumbukumbu

Zifuatazo ni video fupi za tukio hilo.