Pages

AAAAAAAAAAAA

AAAAAAAAAAAAA
Jumatatu, 28 Machi 2016

Wakristo wa kanisa anglikana Majohe wawatembelea watoto yatima Buza

Bibi Mzuri akiingia kwenye basi, akifuatiwa na Mama Joyce tayari kwa kuanza safari kuelekea Buza wakitokea Majohe kanisani.

Wakristo wa kanisa anglikana Mtakatifu Mathayo Majohe leo wamefanya ziara kwenye kituo cha watoto yatima Valentine Chidren's home kituo  kinachofadhiliwa na Askofu Dr Valentino Mokiwa wa kanisa Anglikana Dayosisi ya Dar-es-salaam na wahisani kutoka nchi za nje. Wakristo hao wa Majohe ambao waliongozwa na Padre Patrick Challo walipata muda wa kuongea machache na yatima hao pamoja na uongozi wa kituo hicho. Pia waliwapa watoto hao zawadi za vinywaji baridi, nguo na fedha taslim sh. 380,000/= 
Waliokaa kwenye mkeka ndiyo watoto Yatima wa kituo hicho, wakiwa pamoja na wakristo wa kanisa anglikana Majohe baada ya kuwasili.
 Akina mama wa Umaki Majohe nao pia walishiriki ziara hiyo. Wa kwanza ni Mama Semainda, akifuatiwa na Bibi Mzuri.

Padre Meshack Malilo kushoto wa Mt. Benard Yombo Buza na Padre Challo wa Mt. Mathayo-Majohe wakiimba katika tukio hilo. Ikumbukwe kwamba Padre Malilo ndiye atakayehamia Majohe baada ya Padre Challo kuondoka tarehe 17 April 2016 kwenda Tabata Kisukuru.
 Sala fupi

 Sister Lucy ambaye ndiye Mlezi wa kituo hicho akieleza machache kuhusu kituo
 Baadhi ya wakristo wa Majohe wakiwa wamekaa pamoja na watoto yatima kwenye mkeka, yote hii ni katika kuwafariji watoto hao.
 Watoto yatima wakiimba mbele ya wageni
 Padre Challo akitoa maneno machache
 Mama Mitti aliyesimama, ambaye ni mwenyekiti wa fellowship ambao ndiyo waliosimamia ziara hiyo akitoa maneno machache
Bibi Mzuri akitoa maneno yake kwa niaba ya kikundi cha UMAKI Majohe