Pages

AAAAAAAAAAAA

AAAAAAAAAAAAA
Jumamosi, 16 Aprili 2016

Mkristo wa wiki (ADELA JOHN)


Adela John ndiye aliyebahatika kutufungulia kipengele hiki cha "Mkristo wa Wiki". Nia ya kipengele hiki ni wakristo kufahamiana zaidi. Uwanja ni wenu kumuuliza maswali au kutoa maoni ya HEKIMA. 

Jinsi ya kutuma swali/maoni yako:-
 1. Andika swali/oni lako kwenye sehemu ya Kuchapisha maoni 'textarea' hapo chini.
 2. Chagua unataka kutoa maoni kama nani, kwenye sehemu ya 'Toa maoni kama'.Kama ukituma kwa kutumia akaunti ya Google, basi utatakiwa kuingiza 'email address' na 'password' yako ya google. 
 3. Kama hukumbuki 'email address' na 'password' yako ya google basi chagua kutuma maoni kama 'Asiyejulikana', hapa hutatakiwa kuingiza email address wala password, ila kwenye swali/oni lako andika na jika lako kwa chini ili tujue nani katuma hilo swali au oni.
 4. Bofya kitufe cha 'Chapisha' ili kutuma swali/oni lako.

Angalizo: Kila swali litakaloulizwa lazima lihakikiwe kabla ya kuruhusiwa kuonekana. Hivyo ukishatuma swali lako utalazimika kusubiri lihakikiwe ndipo lionekane kwenye ukurahasa huu.

Endapo utahitaji msaada wowote kuhusu kutuma swali au kujibu swali usisite kuuliza kwa namba hii 0758 3033330 kwa msaada zaidi.

Maoni 19 :

 1. Dada Adela hongera kwa kuwa wa kwanza katika kipengele cha Mkristo wa wiki. Ulijifunza wapi kuimba nyimbo za injili? Maana huwa ninavutiwa na uimbaji wako.

  Mimi ni Mkristo wa Majohe

  JibuFuta
  Majibu
  1. Amina mpendwa wangu.Nashkuru kwa swali: kwa kweli kwa habari ya uimbaji sjapata kujifunza popote isipokuwa ni namna ambavyo Mungu alivyochagua kunipa kipawa cha aina hii ya uimbaji. Ubarikiwe Sana ndugu yangu ktk Kristo. Namba yangu ni 0653801952.

   Futa
 2. Mbona leo hujaja ibadani?

  JibuFuta
  Majibu
  1. Shalom. Amina,ni kweli mpendwa sikuweza kufika ibadani,ni kwasababu za kiafya!nikashindwa kuhudhuria.

   Futa
 3. Sawa mdadaaa, haya niambie ungependa kuolewa na mwanaume mwenye tabia zipi?

  JibuFuta
  Majibu
  1. Shalom.amina asante Sana kwa swali Dada yangu mpendwa.Kwa kweli Awe ni Mwenye kumpenda na kumweshimu Mungu(wokovu ndani yake),mwenye kujiheshimu na kuheshimu huduma na utumishi ambao Mungu ameweka ndani yangu,awe mwenye kupenda kanisa na kujua thamani yake.mwenye kupenda hekima,muelewa na kunia mamoja ktk Neno LA Mungu ambalo tunaongozwa kwalo. Ubarikiwe Sana Dada yangu.

   Futa
 4. 1. Kitu gani Bwana alikutendea ambacho hutakisahau maishani mwako?
  2. Unadhani ni kwa asilimia (%) ngapi unatenda yale yampendezayo Bwana?

  JibuFuta
  Majibu
  1. Shalom kaka yangu mpendwa.asante kwa maswali: kwa kweli ni mengi Mungu amenitendea siwezi kuyasahau maisha ni kwangu.ila lililo kubwa;siwez kusahau jinsi nlivyoishi maisha mabovu,ya dhambi,marafik wasiofaa,mahusiano ysiyofaa na hata kukaa karibu na shimo LA mauti.lakin Leo ninamtukuza Mungu maana Aliniokoa kutoka huko,aliniokoa Mungu hata sasa nayaona hayafai! Kwa habari ya asilimia siwez jihesabia yote,ila naamini na bado naendelea kuisihi neema ya Mungu kuzid kunijalia kutenda mema Sana hata zaidi na zaidi ya hapa.ubarikiwe Sana MTU wa Mungu.

   Futa
 5. Kumtumikia mungu kuna faida, jitahidi dada yangu, ukristo umekupendeza sana..

  JibuFuta
  Majibu
  1. Shalom.amina nashkuru kwa ushauri wako mpendwa wangu.ni kweli kumtumikia Mungu kuna faida!asante Sana MTU wa Mungu. Ubarikiwe

   Futa
 6. Bwana asifiwe Dada Adela, una mpango wowote wa kuimba kama Solo Artist? Na baadae kutoa album yako binafsi

  JibuFuta
  Majibu
  1. Shalom.asante kwa swali mpendwa wangu! Kwa kweli Ninayo maono ya kuimba Kama solo artist,na badae kuandaa albamu yangu! Hivyo nipo mbioni kuelekea na kukamilisha mpango huo.ni kuendelea kuniombea pia,maana maombi ndio msingi wa kufanikisha maono mema ya MTU wa Mungu. Ubarikiwe sana

   Futa
 7. Unaweza kuigiza?

  JibuFuta
  Majibu
  1. Shalom. Asante kwa swali! Ninaweza kuigiza na ninapenda pia.asante

   Futa
 8. Una miaka mingapi? Una level gani ya elimu? Unajishughulisha na nn kwa sasa?

  JibuFuta
  Majibu
  1. Asante. Nina miaka 24,Nina elimu ya form four na ninafanya kazi chini ya mkataba kwa sasa.ubarikiwe

   Futa
 9. 1. Katika akina mama/akina dada wote ambao wameandikwa kwenye biblia unamadmire yupi?

  2. Katika albam yenu ni wimbo upi unaupenda sana? na kwa nini?

  JibuFuta
 10. Shalom,asante! Ktk biblia nabarikiwa Sana mtumishi wa Mungu dorkas ambaye alifanya kazi nzuri,na alipenda kujitolea pia Sana kwa ajiri ya Mungu,na alikumbukwa na Mungu na hata jamii iliyokuwa ikiishi naye na kujua mchango wake. katika ALBAMU YETU YA SAYUNI KWAYA,naupenda na nabarikiwa Sana na wimbo unaoitwa "roho itendayo dhambi". Wimbo huu kila nnapoutafakari huwa nalia na kuguswa Sana,Maana unayahubiri maisha ya MTU ambaye haoni hata thamani ya kumrudia Mungu,istoshe hatutabebeana uovu si baba si mwana.kwa kweli dunia imebadilika Sana inaelekea kubaya na hali mbaya watu wanahubiriwa hawasikii,wakat mwingine hata waimbaj mwenyewe wimbo unatuhubiri lakin wengine wanaimba mzaha na wanafanya maovu bado sirini. Oooh Mungu atusaidie Sana asante

  JibuFuta
 11. Hongera kwa kuwajibu maswali yao UBALIKIWE

  JibuFuta