Pages

AAAAAAAAAAAA

AAAAAAAAAAAAA
Jumapili, 10 Aprili 2016

Picha 10 za ushuhuda wa Muhubiri wa leo juu ya "Utoaji wa Maumivu"

Bw. Manase Machapula toka kigango cha Viwege ndiye aliyetulisha neno la Bwana leo. Pamoja na mengi aliyohubiri, pia alisisitiza juu ya suala la utoaji “Utoaji wa maumivu”, yaani utaoaji wa sadaka ya kumpendeza Mungu ambayo itazaa matunda kwako. Ndipo akatoa ushuhuda wake kupitia picha zifuatazo. Kabla ya kuendelea kusoma ushuhuda hapo chini, tambua kwamba Bw. Manase ni fundi tiles mzuri sana.
 


"Ngoja niwape ushuhuda mmoja. Siku moja nilikua kanisani nikiwa nina sh. 20,000 mfukoni. Ulipofika wakati wa matoleo, nikatoa sh. 5,000 na kubaki na sh.15,000 mfukoni. Kuna sauti ikawa inaniambia nitoe na hizo zilizobaki lkn moyo ukawa unasita kwa sababu ndiyo hela pekee niliyokua nimebaki nayo..."
"Basi nikiwa naiuliza sauti hiyo, hela IPI ambayo unataka nitoe??? Ikasisitiza ni hiyo iliyopo mfukoni. Baada ya kutafakari, kwa unyonge nikainuka taratibu nikaenda kutoa ile 15,000 na kubaki sina hata sh. 1"
"Nilipokua nikitoa ibadani huku nikiwa nina mawazo makali juu ya kupata fedha ya kutumia siku hiyo...."

"Mara nikagongana na mtu njiani, tulihitilafiana kwa muda akitaka kupigana nami sababu nimemgonga, lakini mwishoni yaliisha na mimi nikaendelea na safari".
 "Nilipoachana na yule Bwana, mara nikasikia simu inaita. Nitakapokea...."
 "Kumbe alikua ni mteja ambaye alikua anahitaji kuwekewa tiles kwenye nyumba yake. Nikajua sadaka ya maumivu niliyoitoa inaanza kuleta matunda. Basi kuna sauti ikawa inaniambia kuwa nitaje bei kubwa..."
 "Ndipo nilipoamua kutamka laki 6 kama gharama nzima ya matengenezo, mteja alikubali bila kupinga. Nilitamani ningetaja zaidi ya hiyo. Mteja huyo aliniongezea 50,000/- ikawa 650,000/- na akanipa advance ya sh. 100,000/-"
 "Kama unaamini utoaji wa maumivu una faida nyanyua mkono juuuuuuu"


0 maoni:

Chapisha Maoni