Pages

AAAAAAAAAAAA

AAAAAAAAAAAAA
Jumapili, 10 Aprili 2016

UMAKI-Anglikana Mt.Mathayo-Majohe wamtembelea Mwinjilisti Mbago na Familia yake huko Nzasa

Akina mama wa UMAKI kanisa Anglikana Mt.Mathayo-Majohe wamtembelea Mwinjilisti Mbago na Familia yake huko Nzasa ambapo ndipo anahudumu siku hizi baada ya kuhamishwa toka Majohe. Akina mama hao walipata fursa ya kushiriki ibada pamoja na wakristo wa Nzasa. Kwa mujibu wa taarifa toka kwa akina mama hao, muamko wa waumini wa Nzasa bado ni mdogo. Hivyo kanisa lina waumini wachache sana. Changamoto nyingine ni hali ya jengo la kanisa isiyoridhisha, kwani halina hata mlango na viti havitoshelezi mahitaji. Nyumba anayoishi mtumishi mbago na familia yake ni changamoto nyingine. 

Akina mama hao waliipatia familia ya Mwinjilisti Mbago zawadi mbalimbali kama picha zinavyoonesha hapo chini.

Mwinjilisti mbago akihubiri wakati wa ibada
 Sala ya mwisho baada ya ibada

Zifuatazo ni picha za kuikabidhi zawadi familia
 Mama Mitti akikabidhi zawadi.
 Mama Mwimbe akikabidhi zawadi

 Mama Wawili akikabidhi zawadi
Mama Joyce akikabidhi zawadi
 Ni furaha tu

Sala ya kufunga


Maoni 2 :