Pages

AAAAAAAAAAAA

AAAAAAAAAAAAA
Jumamosi, 21 Mei 2016

Mkristo wa wiki (John Mwimbe)


John Mwimbe (Katibu wa Kanisa) ndiye "Mkristo wa Wiki". Uwanja ni wenu kumuuliza maswali au kutoa maoni ya HEKIMA. 

Jinsi ya kutuma swali/maoni yako:-

 1. Andika swali/oni lako kwenye sehemu ya Kuchapisha maoni 'textarea' hapo chini.
 2. Chagua unataka kutoa maoni kama nani, kwenye sehemu ya 'Toa maoni kama'.Kama ukituma kwa kutumia akaunti ya Google, basi utatakiwa kuingiza 'email address' na 'password' yako ya google. 
 3. Kama hukumbuki 'email address' na 'password' yako ya google basi chagua kutuma maoni kama 'Asiyejulikana', hapa hutatakiwa kuingiza email address wala password, ila kwenye swali/oni lako andika na jika lako kwa chini ili tujue nani katuma hilo swali au oni.
 4. Bofya kitufe cha 'Chapisha' ili kutuma swali/oni lako.

Angalizo: Kila swali litakaloulizwa lazima lihakikiwe kabla ya kuruhusiwa kuonekana. Hivyo ukishatuma swali lako utalazimika kusubiri lihakikiwe ndipo lionekane kwenye ukurahasa huu.

Endapo utahitaji msaada wowote kuhusu kutuma swali au kujibu swali usisite kuuliza kwa namba hii 0758 303330 kwa msaada zaidi.

Maoni 9 :

 1. Bw.John ikitokea wakristo waruhusiwe kuoa wake wanne utafurahi ama la? kwa nini?

  JibuFuta
  Majibu
  1. Wakristo hatutaruhusiwa kuoa wake zaidi ya mmoja labda biblia iandikwe upya

   Futa
 2. Katibu tujuze changamoto mbili kubwa unazozipata katika kazi yako ya Ukatibu.

  JibuFuta
 3. 1. Matoleo yapo chini sana kwa hiyo inaleta ugumu katika utendaji
  2. Mahudhurio hafifu ya wanajumuiya kwenye ibada za jumuiya zao

  JibuFuta
  Majibu
  1. - Unadhani nini sababu za matoleo kuwa chini sana na mahudhurio hafifu kwenye jumuiya?
   - Je, changamoto hizo zilikuwepo toka muda mrefu? Au ziliibuka muda hivi karibuni?

   Futa
  2. 1. Nafikiri hali ya uchumi jinsi ilivyo kwa sasa au ugumu wa waumini wenyewe na pia kukosa semina au mafundisho sahihi ya utoaji

   2. Uhafifu wa mahudhurio kwenye ibada za jumuiya kuna sababu nyingi sana ambazo si vema kuziongelea hapa. Hizi changamoto za mahudhurio zimeanza muda mrefu sana ila kwa sasa imekuwa maradufu

   Futa
 4. Hongera John kwa kuwa mkristo wa wiki. Una mpango wa kuwa na watoto wangapi katika familia yako. Au 11 kama timu ya soka?

  JibuFuta
  Majibu
  1. asante sana. Mimi sina idadi yoyote ambayo nimepanga ila nitakaojaaliwa kupata nitamshukuru Mungu

   Futa
  2. Kama ni hivyo basi tunakuombea Mungu akujaalie ugonge copy kama 24 hivi hahahahaaaa

   Futa