Pages

AAAAAAAAAAAA

AAAAAAAAAAAAA
Jumapili, 15 Mei 2016

Picha 18: Watoto Aron na Nasho wakipambana kwa staili za kumsifu Bwana kwa kucheza

Kushoto ni Nasho na Aron kulia wakichuana vikali katika kumsifu Bwana kwa kucheza na kuimba. Wakali hawa wa styles za kucheza nyimbo za kumsifu Bwana ni waimbaji wa Uinjilisti Kwaya. Mpambano uliendelea kama ifuatavyo.
 Aron alianza taratibuuu, huku akionekana kumsoma mpinzani wake
 Nasho naye alianza kwa staili ya kibabe, akitunisha kifua ili kumtisha mpinzani wake.
 Aron akaona isiwe tabu, ili kuepuka kutishwa na kifua cha Nasho aligeuka upande mwingine
 Nasho naye akajibu mapigo kwa kugeuka upande wa mwingine. Mchuano ukaendelea...
 Duuh! Kweli damu nzito kuliko maji, mdogo wa Aron (Albert) aliamua kuja kumtunza kaka yake ili ampe nguvu ya kuendelea na mpambano.
 Nasho kama vile alinywea kidogo, baada ya kuona kuna hujuma imeanza kutokea. Iweje mwenzake apewe zawadi. Ila akakaza moyo na kuendelea na pambano hivyo hivyo.
 Baada ya kutiwa moyo kwa zawadi Aron akaongeza nguvu, na tabasamu likaonekana sasa. Pambano likaendela.
 Nasho akakazana, hii nadhani ni bodaboda style.
 Aron anaonekana kama amevutiwa na bodaboda style, naona kama anaigilizia sasa
 Nasho akaongeza madoido, hii sijui hata ni staili gani
 Hee! Aron akazinduka. Akaja na staili yake ya mikono juu
 Nasho akacopy na kupaste staili ya mikono juu. Hii hatari sasa
 Aron akiangalia kwa uchungu baada ya staili yake ya mikono juu kuibwa hahaahhahaa
 Duuh! Nasho kabadili staili, hizi ni ngumi sasa
 Aron kanywea baada ya kuona ngumi. Si unamuona kashusha mikono yake chini hahahahahha
 Ohoooo! sasa ni kutishana live live. Kila mtu akimuonya mwenzake asiibe staili
Ohoooo! kuchinjana tena??? 

Mimi sikutaka ushahidi, nikaamua niache kupiga picha. Kilichoendelea baada ya hapo sijui.

UNADHANI NANI MSHINDI KATI YA ARON NA NASHO???

Maoni 3 :

 1. Amaweli mpambano ulikuwa mkalii

  JibuFuta
 2. Wametisha sana, nani alishinda sasa?

  JibuFuta
  Majibu
  1. Katibu nyie (waumini) ndiyo majaji.Inabidi kila mtu aseme nani kashinda kati ya wababe hao teh teh

   Futa