Pages

AAAAAAAAAAAA

AAAAAAAAAAAAA
Jumapili, 17 Julai 2016

Picha 10: Mbwembwe za wazee(vijana) wa kanisa waliosimamia ibada ya pili leo


Leo tulibahatika kusimamiwa na wazee(vijana) wa kanisa Jacob (kushoto) na Allen (kulia). Kwanza ninawapongeza kwa moyo wao wa kujitoa kumtumikia Bwana angali vijana wadogo. Ni vijana wachache sana wanaojitoa kumtumikia Bwana katika karne hii. Mbarikiwe sana Jacob na Allen. Pamoja na kujitoa huko lakini usimamizi wao ulienda sambamba na kujisahau kidogo, si unajua vijana wana mambo mengi. Endelea kutazama picha zifuatazo ufahamu nini kilitokea.
Hapa Allen akisimamia zoezi la utoaji sadaka. Kama vile kanuna hivi, sijui nini kilimsibu. Nway...nadhani alikuwa anatafakari neno la Bwana kwa kina hadi akaonekana kama kanuna.
  Huyu ni Jacob ambaye alikuwa akisaidiana na Allen kusimamia zoezi la utoaji sadaka.
Hapa Jacob akiwaongoza waumini kwenda kushiriki meza ya Bwana
Hapa wakiwa makini sana na kazi yao, wakiwa wamesimama nje ya kanisa huku wakitazama ndani kwa umakini mkubwa kuhakikisha hakuna kinacho haribika.

Baada ya hapo vimbwanga vikaanza, sijui walukuwa wamechoka? Maana walishiriki pia ibada ya kwanza kumsifu Bwana wakiwa na kwaya ya Sayuni
Jacob akiwa nje akaamua kukaa zake chini huku akionekana kama anawaza mbaliiiiii. Yani hapo network ilihama kabisa na kujisahau kama yupo kanisani na ni mzee(kijana) wa kanisa wa zamu.
Stori zikaendelea, pichani wanaonekana wakisalimiana na rafiki yao ambaye alikuwa akipita njia karibu na kanisa.
Mama yangu!! wakakaa chini kabisa wakiendelea stori. Aisee wamesahau kabisa kwamba kuna kusimamia ibada.
Ohoooo! wakaanza kupigana picha kabisa. Walioweka pozi ni Elikana na Jacob, mpiga picha ni Allen. Kazi kweli kweli hahahhaaaaaa.
Ghaflaaa! wanashtushwa na sauti ya Katibu wa kanisa John Mwimbe (mlangoni) akiwakumbusha kupeleka chombo cha sadaka maalum haraka. Hapo ndipo Jacob akakurupuka toka kwenye pozi la kupiga picha na kuanza kutafuta chombo cha sadaka. Mtazame jicho lilivyo mtoka hahahaahaahaaa. Hata huko anapoelekea chombo hakikuwepo.
Ikabizi azame ndani ya kanisa mbio mbio kukitafuta chombo cha sadaka. Kilichoendelea humo ndani mimi sijui teh teh teh.

Ila tunawashukuru sana kwa moyo wao wa kujitoa kusimamia ibada ya pili licha ya kushiriki pia ibada ya kwanza.

0 maoni:

Chapisha Maoni