Pages

AAAAAAAAAAAA

AAAAAAAAAAAAA
Jumatatu, 1 Agosti 2016

Anglikana-Majohe yaichakaza KKKT-Majohe 1-0, vituko vyatawala

Kikosi cha Kanisa Anglikana Mt. Mathayo-Majohe Dsm wakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya mchezo kuanza. Waliosimama kulia ni Mfadhili wa timu Elikana Kipala, na mwenye jezi ya Yanga ni Mwalimu wa timu John Mwimbe ambaye pia ni Katibu wa kanisa. Hadi refa anavunja mchezo, Anglikana walikuwa wanaongoza kwa goli 1-0, goli lililofungwa na Isdory Maximilian.

Mchezo ulitawaliwa na vituko vya hapa na pale
  • Dismas (mwenye bukta nyekundu, waliochuchumaa) alijigamba sana kabla ya mchezo kwamba yeye ni namba 8 hatari sana. Cha ajabu alicheza kwa dakika 15 tu akaanza kuhema juu juu kama perege. Na kuamua kuomba kutoka mwenyewe hahahahahaaaa.
  • Mipira miwili ilipasuka na kupelekea mchezo kuvumjika dk ya 70, lkn hadi muda huo Anglikana walikuwa wanaongoza kwa goli 1.
  • Uwanja uliotumika ulikuwa una shimo kubwa katikati, hali iliyopelekea wachezaji kuzama hadi usawa wa kiuno wakiwa eneo hilo.
A
Watazamaji wakiufuatilia mchezo kwa makini

Maoni 2 :

  1. Hao wachezaji wa kucheza dk.15 inabidi wachunguzwe kabla hawajawa majibu.

    JibuFuta
  2. Hahahahaaa naona una utani na bro Dismas. Nasikia kaanza mazoezi kwa nguvu zote kwaajili ya mchezo ujao

    JibuFuta