Pages

AAAAAAAAAAAA

AAAAAAAAAAAAA
Jumapili, 7 Agosti 2016

Mnada wa kanga na kikoi

Mwisho wa Ibada ya leo kulifanyika mnada wa Kanga na Kikoi ambavyo mkristo alivitoa kama sadaka. Pichani juu ni Mnadishani (Ndaison) akiwa na kikoi mkononi na mkusanya fedha wakiwa tayari kuanza mnada huo.
 Mkusanya fedha akiwa tayari kukusanya fedha
 Muonekano halisi wa kikoi hicho
Padre Malilo ndiye aliyefanikiwa kukipata kikoi hicho baada ya kununuliwa na baadhi ya waumini, hasa wana kwaya wa Paradiso toka Buza ambao walishiriki ibada pamoja nasi leo. Pichani anaonekana Mwinjilisti Haule akiikunja kanga hiyo ya Padre Malilo
 Kanga ikioneshwa kwa waumini kabla ya kuanza kuinadi.
Hatimaye Mwinjilisti Yohana Lenda (kulia) akipongezwa na Elikana baada ya kufanikiwa kuipata Kanga hiyo.

0 maoni:

Chapisha Maoni