Pages

AAAAAAAAAAAA

AAAAAAAAAAAAA
Jumapili, 7 Agosti 2016

Ujio wa Paradiso Kwaya watubariki sana wana Anglikana Majohe

Leo tumetembelewa na Paradiso Kwaya toka Kanisa Anglikana Mt. Benard Buza Dar es Salaam. Waumini wa hapa Majohe tumebarikiwa sana na ujio wao. Uwezo wao mkubwa wa kumsifu Bwana kwa njia ya uimbaji ni moja ya sababu ya kubarikiwa na ujio wao. Licha ya kushiriki nasi katika ibada ya asubuhi, pia watashiriki nasi kwenye mkutano wa injili wa leo ambao utafanyika hapa kanisani kuanzia saa 8:00 mchana. Mbarikiwe sana na karibuni tena siku nyingine.
Mwenyekiti msaidizi wa Paradiso Kwaya dada Sophia Paul akimaliza kuwasalimia waumini wa hapa Majohe kwa niaba ya kwaya yake
Wakijiandaa kuimba
Wakijiandaa kuimba
Wakiimba
Wakitoka nje mwisho wa ibada
Wakitoka nje mwisho wa ibada


0 maoni:

Chapisha Maoni