Pages

AAAAAAAAAAAA

AAAAAAAAAAAAA
Jumapili, 2 Oktoba 2016

Kwa mara ya tano mfululizo jumuiya ya Yakobo yaitwaa kombe la Sikukuu ya Mtakatifu Mathayo

Kwa mara ya tano mfululizo Jumuiya ya Mtakatifu Yakobo imefanikiwa kutwaa kombe la sikukuu ya Mtakatifu Mathayo baada ya kuzibwaga jumuiya nyingine saba. Ushindi huu umepatikana baada ya jumuiya hiyo kukusanya kiasi kikubwa cha sadaka ya Sikukuu ya Mtakatifu Mathayo kuliko jumuiya nyingine.

Pichani juu ni Mama Miti mwenyekiti wa jumuiya ya Yakobo akinyoosha kikombe juu baada ya kukabidhiwa.

Mama Miti akiongea machache akiwa na wanajumuiya wenzake wa Yakobo
Mama Miti akikabidhiwa kikombe na Padre Meshack Malilo
Mama Miti akiwa pamoja na meza kuu, toka kulia ni Mwinjilisti Haule, John Mwimbe (Katibu), Padre Malilo na John Lugendo (Mshauri wa Padre)

Maoni 1 :

  1. Hongereni sana mt. Yakoba mungu azidi kuwabariki kazi yenu si bure

    JibuFuta