Pages

AAAAAAAAAAAA

AAAAAAAAAAAAA
Jumapili, 4 Desemba 2016

Igizo la watoto lakonga nyoyo za waumini, pata stori yake katika picha 9

Watoto walithibitisha kuwa wana uwezo wa kuigiza kupitia igizo lao ambalo lilikonga sana nyoyo za waumini. Ingizo hili lilihusu familia mbili ambapo, moja ilikuwa ikimtegemea Mungu kwa kusali kabla ya kulala na nyingine ilikuwa ikimtegemea Mganga wa kienyeji. Pichani juu ni familia inayomtegemea mganga wa kienyeji ikiwa imealala bila hata kumuomba Mungu awalaze salama.
Pasipo na Mungu shetani hutawala. Pichani mchawi anaonekana akiwaloga wana familia ambao hawana utaratibu wa kusali kabla ya kulala.
Mchawi alifanikiwa kumchukua mtoto mmoja wa familia hiyo na kwenda kumlaza nje ya nyumba pasipo mtoto wala mwana familia kutambua.
Kushoto ni mtoto ambaye amelazwa nje ya nyumba na Mchawi. Kulia ni Mama wa mtoto na dada wakishangaa kutomuona mtoto wa kiume ndani. Waliamua kumtafuta na kumkuta kalazwa nje...
Baada ya kumkuta mtoto wao nje, waliamua kwenda kwa mganga kwani walijua watakuwa wamelogwa na majirani. Ndipo mganga alipowapa dawa na kwenda kuinyunyizia kwa jirani yao ambayo ni familia inayomtegemea Mungu.
 Waumini wakifuatilia igizo kwa umakini mkubwa
Pichani ni familia inayomtegemea Mungu, hapo wakiomba kabla ya kulala. Hii ndiyo familia iliyohisiwa kumloga mtoto ambaye alilazwa nje na mchawi
Mchawi (aliyekaa chini) alijaribu pia kwenda kuiloga familia ambayo inamtegemea Mungu. Kwa nguvu za Mungu alinasa hapo hapo mlangoni na kukutwa na wenye nyumba kama anavyoonekana pichani akiwa chini.
Familia inayomtegemea mganga ilikuja kwa jirani yao na kukuta mchawi akiwa amenasa mlangoni. Baada ya familia ya Mungu kuanza kufanya maombi ya kumkemea mchawi, maombi hayo yaligusa hata ile familia inayomtegemea Mganga wa kienyeji na kupelekea wote kuanguka chini kama waonekanavyo pichani.

Mwisho wa igizo

0 maoni:

Chapisha Maoni