Pages

AAAAAAAAAAAA

AAAAAAAAAAAAA
Jumapili, 19 Machi 2017

'Parish Worker' wetu anastahili pongezi katika hili

 
Si rahisi kwa mwandishi wa habari hii kufahamu ufanisi wa kila kitu afanyacho ‘Parish Worker’ wetu hapa kanisani Bw.  Allen Vicent, lakini kwa kile akifanyacho kwenye usimamizi mzuri wa kadi za sadaka/matoleo hakika anastahili pongezi kubwa sana.
Kabla ya kuteuliwa kwake kuwa ‘Parish Worker’, waumini tulipata tabu sana katika suala zima la kadi za matoleo. Yafuatayo ni baadhi ya mapungufu ambayo amekuwa akiyafanyia kazi  kikamilifu tangu alipoanza kazi tarehe 12 Juni 2016.
  • Kupotea kwa kadi
  • Kuchanganyika kwa kadi
  • Kukosa usaidizi wakati wa kutafuta kadi n.k
Matatizo tajwa hapo juu yalikuwa ni kikwazo sana kwa waumini ambayo yalipelekea baadhi ya yao kutumia muda mrefu kutafuta kadi na kupelekea kuchelewa kuingia ndani ya kanisa kwaajili ibada. Wengine walilazimika kutoa sadaka bila bahasha baada ya kuzikosa.
Hakika kwa sasa matatizo kuhusu kadi yamekoma, Parish Worker amekuwa akionesha ushirikiano mzuri sana kwa waumini katika saula zima la kadi za matoleo.
Atambue kwamba bidii yake inaonekana na Mungu ambariki sana.

0 maoni:

Chapisha Maoni