Pages

AAAAAAAAAAAA

AAAAAAAAAAAAA
Jumanne, 16 Mei 2017

Utabiri wa Padre Malilo juu ya Ubingwa wa Yanga watimia kwa 99%

Kama ulikuwa mmoja wa waumini walioshiriki ibada za tarehe 26/02/2017 utakumbuka jinsi waumini washabiki wa Yanga na Simba walipotoa sadaka kufuatia mchezo(25/02/2017) wa watani hao ambao uliisha kwa Simba kushinda 2-1.

Katika kudumisha utani huo wa jadi, Padre Malilo aliwaomba waumini washabiki wa Simba na Yanga watoe sadaka, na alitabiri ambao watatoa sadaka nyingi zaidi timu yao itakuwa bingwa wa kombe la ligi 2016/2017 (VPL). Waumini washabiki wa Yanga walifanikiwa kutoa sadaka nyingi zaidi ya Simba.

Hivyo utabiri wake umetimia leo kwa 99%, ambapo timu ya Yanga imefanikiwa kukaribia kutwaa kombe la ligi kuu Tanzania (VPL) baada ya kuifunga timu ya Toto Africans 1-0 na kufikisha pointi 68 na magoli 57. Endapo Simba atashinda mchezo wake wa mwisho dhidi ya Mwadui atafikisha pointi 68 lakini inatakiwa kufunga magoli 13-0 ili kuifikia Yanga kwa magoli. Pia ili hilo lifanikiwe inabidi Yanga wapoteze mchezo wao wa mwisho na Mbao FC. Kwa kuzingatia hayo, utagundua ni vigumu kwa Yanga kutokuwa mabingwa mwaka huu.

Naweza kusema utabiri wa Padre Malilo umetimia.

0 maoni:

Chapisha Maoni