Pages

AAAAAAAAAAAA

AAAAAAAAAAAAA
Jumapili, 20 Agosti 2017

Bibi Mzuri ahamasisha utoaji ili kupata posho za watumishi

Kwa niaba ya Kamati Tendaji ya Mtaa, leo ibada ya pili Bibi Mzuri (Mshauri wa akina mama) alihamasisha utoaji wa sadaka ili tuweze kuwatunza watumishi wa mtaa wetu. Kwa sasa mtaa una hali mbaya sana kufuatia kupungua sana kwa matoleo ya waumini. Pamoja na kuhamasisha, waumini waliombwa kuahidi kiasi ambacho wanaweza kukitoa kila mwisho wa mwezi kwaajili ya posho ya watumishi. Zoezi hili litadumu kwa muda wa miezi mitatu. Baadhi ya waumini waliitikia kwa kuahidi jinsi walivyoguswa.

Zoezi hili lilifanyika pia ibada ya kwanza ambapo mshauri wa akina Baba (George Lugendo) alihamasisha pia.

Mungu atubariki katika kufaikisha hili.

0 maoni:

Chapisha Maoni