Pages

AAAAAAAAAAAA

AAAAAAAAAAAAA
Jumatano, 8 Novemba 2017

'Kanisa la Pombe' laanzishwa Afrika Kusini

Mmoja wa waumini akibatizwa na Askofu Matiki kwa pombe ambayo aliichagua muumini mwenyewe.

Askofu Matiki ameanzisha ‘Kanisa la Pombe’ huko Johannesburg Afrika Kusini. Licha ya kanisa hilo kuanzishwa hivi karibuni lakini limeshajikusanyia waumini 500 ambao wote ni wanaume. Ubatizo wa kanisa hilo hufanywa kwa kutumia pombe badala ya maji. Mbatizwaji huchagua pombe ya aina yoyote aipendayo ili Askofu huyo aitumie kumbatiza. Askofu huyo ameeleza nia ya kuanzisha kanisa hilo ni kuwapa fursa walevi wote ambao hawakubaliki kusali katika makanisa mengine ambayo hupinga unywaji wa pombe.

Chakushangaza kanisa hilo halina nyumba maalum ya ibada (kanisa), waumini pamoja na mchungaji wao hukutana kwenye kilabu chochote cha pombe siku ya jumapili na kufanya ibada kuanzia saa tano asubuhi hadi mchana. 

Askofu huyo alizidi kueleza kwamba, hataki kuwashirikisha wanawake kwa sasa kwenye ibada zake kwa sababu anaifahamu tabia ya wanaume wanapokuwa wamelewa. Wanaweza kuwasumbua wanawake, hata hivyo anaendelea kuwafundisha wanaume hao taratibu jinsi ya kusali na wanawake bila kuwabughudhi hata kama wamelewa.
 Ibada ikiendelea kwenye kilabu cha pombe


Habari hii imetafsiriwa kutoka www.dailymail.co.uk

0 maoni:

Chapisha Maoni