Pages

AAAAAAAAAAAA

AAAAAAAAAAAAA
Ijumaa, 8 Desemba 2017

Picha 6: Pale Bibi harusi alipogeuka na kuwa muuguzi wa msimamizi wake

Agnes kulia akimsimamia Mama Mwimbe wodini baada ya kuumwa tumbo ghafla mara baada ya kuwasili Dodoma kwaajili ya kusimamia harusi ya Dismas na Agnes.

Ikiwa imebaki masaa kadhaa kabla ya harusi ya Dismas na Agnes kufanyika huko Dodoma, Mama Mwimbe ambaye ndiye msimamizi wa harusi hiyo aliugua tumbo ghafla baada ya kufika Dodoma jana saa 1:30 jioni. Aliendelea kuvumilia akihisi ni tumbo la muda mfupi lakini liliendelea kumuuma. Saa 5 usiku alipelekwa hospitali ya Aghakan ambapo alipatiwa matibu na kuruhusiwa baada ya kupata nafuu. Mungu amtangulie apone haraka ili aweze kusimamia harusi hiyo vema, Amina.

 Mama Mwimbe akiwa wodini
 Akitoka wodini baada ya kupata nafuu
Kutoka kulia ni Agnes (Bibi harusi), Mama Mwimbe (Msimamizi), Dismas (Bwana harusi) na John Mwimbe (Msimamizi) wakiwa kwenye picha ya pamoja Hospitali ya Aghakan mara baada ya mgonjwa kupata nafuu.
 Agnes kulia na Mama Mwimbe
Safari kuelekea nyumbani ikitaraji kuanza

0 maoni:

Chapisha Maoni