Pages

AAAAAAAAAAAA

AAAAAAAAAAAAA
Alhamisi, 1 Machi 2018

Afrika Kusini: Mchungaji awapulizia waumini dawa ya kuua wadudu ili kuwaponya


IMANI YA HATARI: Mchungaji wa nchini Afrika Kusini almaarufu kama "Mchungaji wa mateso" aliyekuwa akiwapulizia washirika wake dawa ya kuulia wadudu usoni ameamuriwa na mahakama kulipa faini ili kuepuka adhabu ya kwenda jela.

Lethebo Rabalago amepewa uchaguzi wa adhabu ya kwenda jela miaka minne au kulipa faini ya fedha za Afrika kusini jumla ya randi 21,000 sawa na Dola za Kimarekani 1,800 baada ya kupatikana na hatia ya kushambulia na kukiuka Sheria ya Mazao ya Kilimo.

Mchungaji huyo mwenye miaka 25 amekubali kulipa faini hiyo kwa awamu kwa kutoa randi 3000 kila mwezi, kwa mujibu wa gazeti la Soweto.

Rabalago ambaye anaendesha Kanisa la Mount Zion alikamatwa baada ya kuibuka kwa taarifa za kutumia bidhaa za "kuponya" wafuasi wake kupitia aina mbalimbali za magonjwa yakiwemo saratani na Ukimwi mwaka 2016.

Hata hivyo kesi hiyo ilifunguliwa na waumini watano walioamua kuwaeleza polisi kuhusu kupuliziwa dawa hizo moja kwa moja usoni, huku mmoja akiambulia kukohoa mfululizo kwa zaidi ya mwezi mmoja.Chanzo: AZAM TV

0 maoni:

Chapisha Maoni