Pages

AAAAAAAAAAAA

AAAAAAAAAAAAA
Jumamosi, 17 Machi 2018

Picha 14: Kilichojiri nyumbani kwenye msiba wa Dominic Lucas Peter

Ni vilio na majonzi vilitawala nyumbani kwa marehemu Dominic Peter aliyefariki jana alfajiri baada ya kuanguka ghafla nyumbani kwake Chuo Rada, Majohe-Dar es Salaam. Ibada iliongozwa na Padre Johson Lameck wa Kanisa Anglikana Mtakatifu Mathayo Majohe-Dar es Salaam, huku Padre Patrick Challo akitoa mahubiri mazuri na yenye funzo kubwa kwa waombolezaji. Pia walikuwepo Wainjilisti Sospeter Mrope na John Haule kwenye ibada hiyo. Baada ya ibada mazishi yalifanyika makaburi ya Kwanamtumbo Majohe-Dar es Salaam. Marehemu ameacha mjane na watoto watano. Bwana ametoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe. Amina
Jeneza likiwasili nyumbani
Meza ya watumishi walioongoza ibada: Toka kulia ni Mwinjilisti John Haule, Fr. Johnson Lameck, Fr. Patrick Challo na Mwinjilisti Sospeter Mrope
Katikati mwenye mavai meupe na kilemba cheupe ni Mjane (mke wa marehemu)
Fr. Challo akihubiri
Jeneza likiwa ndani mwa nyumba ya marehemu
Jeneza likiwa ndani mwa nyumba ya marehemu
Mjomba wa marehemu akisoma historia

Picha zifuatazo ni wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa marehemu. Ndugu wa karibu wakionekana kulia kwa uchungu huku wakisaidiwa


0 maoni:

Chapisha Maoni