Pages

AAAAAAAAAAAA

AAAAAAAAAAAAA
Jumapili, 11 Machi 2018

Picha 6: Mchungaji Tuheri asafirishwa kwenda Manerumango kwa mazishi

Ilikuwa tarehe 8/3/2018 Bwana alipomtwaa mtumishi wake Mchungaji Tuheri Aaron wa Usharika wa Magogoni KKKT - Kigamboni. Kifo chake kilitokea usiku kwa ajali ya gari akitokea Mbagala, Dar es Salaam. Waumini na waombolezaji wengine wakiongozwa na Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dkt. Alex Malasusa walipata fursa ya kumuaga leo kwenye ibada iliyofanyika usharikani magogoni KKKT Kigamboni na baadae saa moja jioni kusafirishwa kuelekea Manerumango mkoani Pwani kwa mazishi. Marehemu ameacha mjane na watoto wawili. Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi. Amina
 
 Jeneza likitolewa nje baada ya ibada kanisa KKKT usharika wa Mgogoni-Kigamboni ambapo ibada ya kumuaga Mch. Tuheri ilifanyika leo
Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dkt. Alex Malasusa wa mwisho kulia, akitoka nje ya kanisa KKKT usharika wa Mgogoni-Kigamboni ambapo ibada ya kumuaga Mch. Tuheri ilifanyika leo


Mch. Tuheri enzi za uhai wake

0 maoni:

Chapisha Maoni