Pages

AAAAAAAAAAAA

AAAAAAAAAAAAA
Alhamisi, 15 Machi 2018

Pumzika kwa amani Padre Onesphory Kayombo


Pd. Onesphory Lazaro Kayombo (C.PP.S) (58) pichani juu amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Kinondoni Jijini Dar alikokuwa amelazwa. Padre Kayombo alikuwa akitumika kanisa Katoliki Parokia ya Tegeta-Dar es Salaam.

Padre Kayombo ni tunda la kwanza kabisa la Wamissionari wa Damu Azizi ya Yesu kutoka Manyoni, Singida. Shirika linapoadhimisha Jubilei ya miaka 50 ya uwepo na utume wake nchini Tanzania linamwangalia Padre Kayombo, maarufu kama Kalikenye kwa jicho la pekee. Na kutoka Manyoni, Shirika linaendelea kupata miito ya kimissionari, kielelezo cha ushuhuda wenye mvuto na mashiko! Katika maisha na utume wake, amekuwa ni Paroko na Jaalim Seminari kuu ya Peramiho, Jimbo kuu la Songea.

Tarehe 29/10/2016 alifanyiwa jubilee ya kutimiza miaka 25 ya Upadri katika Parokia ya Kupaa na Bwana, Manyoni-Singida.

Kwa taarifa zaidi kuhusu msiba huu tembelea ukurasa wa facebook wa Radio Maria https://web.facebook.com/radiomaria.tanzania/

Padre Kayombo akiwa na waumini wa Parokia ya Kupaa na Bwana, Manyoni-Singida siku ya kuadhimisha miaka 25 ya Upadri wake.

Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe. Amina

0 maoni:

Chapisha Maoni