Pages

AAAAAAAAAAAA

AAAAAAAAAAAAA
Jumanne, 10 Aprili 2018

Brian Deacon "Niliokoka baada ya kuigiza filamu ya Yesu"

Katika kipindi cha  kuelekea siku kuu ya Pasaka au christmass, ni jambo la kawaida kukuta nyumba za waumini wa dini ya Kikristo zikiwa zimepambwa na picha mbalimbali za Yesu, lakini pia kama wewe ni muumini wa dini hiyo, unapotajiwa au kulisikia jina la Yesu, kuna picha fulani inakujia mawazoni, kuna sura fulani inakujia mawazoni, si picha au sura nyingine, bali ni sura ya Yesu.

Wapo wanaodhani kuwa picha hiyo au sura hiyo ndiyo Yesu mwenyewe aliyezaliwa yapata miaka 2000 iliyopita, hapana, hakuna anayejua sura ya Yesu ikoje, anaonekana vipi, bali mtu huyo ambaye ulimwengu umezoea kumwona kama ndiyo Yesu wa Nazareti, huyu ni jamaa mmoja anayejulikana kwa jina la Brian Deacon, huyu ndiyo jamaa aliyeigiza ile filamu maarufu ya Yesu, inayojulikana kwa jina la ‘Jesus Film’ mwaka 1979. filamu hiyo iliigizwa na watu mbalimbali ambao wengine wapo hai mpaka leo, picha za filamu hiyo zilipigwa nchini Israeli.
Kutoka kushoto ni Dalia Shapira aliyeigiza kama Mary Magdalene, Babi Neeman aliyeigiza kama Yakobo, Niki Mitai aliyeigiza kama Petro na Brian Deacon aliyeigiza kama Yesu katika filamu hiyo
Katikati ndiyo Brian Deacon aliyeagiza kama Yesu, Kushoto ni mmoja wa watoto wa waigizaji katika filamu hiyo aliyeigiza kama Yesu mtoto na kulia alieyeigiza kama Yesu mwenye umri wa miaka 12


Chanzo: http://www.swahili-movies.com

0 maoni:

Chapisha Maoni