Pages

AAAAAAAAAAAA

AAAAAAAAAAAAA
Jumatatu, 9 Aprili 2018

Mchungaji auawa kwa risasi Afrika Kusini

Mchungaji Paul Kamba mwenye uraia wa Uganda ameuawa nchini Afrika Kusini tarehe 4/4/2018 ambapo alikuwa ni Mchungaji Kiongozi wa kanisa lijulikanalo "Destiny Midwives Christian Centre" lililopo Edenvale, Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa Mchungaji Mondo Mugisha ambaye alikuwa rafiki wa karibu wa Mchungaji Kamba, siku ya tukio baada ya marehemu kuhudumu kwenye misa ya asubuhi alielekea ofisini kwake akiwa na mkewe kupumzika. Wakati akitoka ofisini alikutana na wauaji hao ambao walimpiga risasi mbili za tumbo. Baada tukio hilo wauaji hao walitoweka bila kuchukua kitu chochote.

Siku moja baada ya tukio, mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu kuelekea Uganda ilianza kufanywa.

Imetafsiriwa kutoka tovuti ya: https://www.newvision.co.ug0 maoni:

Chapisha Maoni