Pages

AAAAAAAAAAAA

AAAAAAAAAAAAA
Jumamosi, 8 Septemba 2018

TANZIA: Peter Mwingereza ametutoka leo

Mtaa wetu umepata msiba kwa kuondokewa na mwanajumuiya wa Jumuiya ya Mt. Mariam, Peter Mwingereza (pichani) aliyefariki usiku wa kuamkia leo hospitali ya Kisarawe alipokuwa amelazwa. Ibada ya mazishi itafanyika nyumbani kwake (Majohe, Kwa Meddo) kesho (9/9/2018) mchana na kufuatiwa na mazishi saa 10 jioni makaburi ya Pugu-Dsm. BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.

0 maoni:

Chapisha Maoni