Pages

AAAAAAAAAAAA

AAAAAAAAAAAAA

Taarifa fupi ya Kanisa

.
1. Utangulizi
Kanisa Anglikana Mt. Mathayo Majohe lilianzishwa mnamo tarehe 13/12/1999 na idadi ya waumini wasiozidi kumi (10) na ibada ilikuwa ikifanyika nyumbani kwa muumini mmojawapo, idadi ya waumini iliongezeka siku hadi siku. Mwaka 2005 kilinunuliwa kiwanja cha kanisa ambacho taratibu zinaendelea kufanyika kupata hati miliki, pia kuanzia wakati huo baada ya kununua kiwanja hicho ulianza ujenzi wa kanisa la muda ambalo leo hii tulifanyia misa lakini pia ibada ya kwanza ilifanyika tarehe 07/01/2007 ikiwa ni Jumapili ya mwanzo kwa mwaka huo na idadi ya waumini ilifikia hamisni na nane (58).

2. Waumini
Kanisa lina idadi ya waumini wanaofikia mia tatu kumi na sita (400) kati yao, wanaume ni tisini (100) wanawake ni mia moja kumi na mbili (160) na watoto ni mia moja arobaini na nne (140).

3. Uongozi wa Kanisa
Kanisa lina jumla ya viongozi ishirini na (27) wanaounda halmashauri kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2011 mpaka mwaka 2016 na kufanya vikao kufuatana na Almanac lakini pia kufanya vikao vya dharura pale linapojitokeza jambo la ulazima wa kukutana, vile vile zipo kamati mbalimbali zinazofanya kazi kutokana na mahitaji husika ya kanisa. Kwa sasa kanisa linaongozwa na Padre Johnson Lameck, akisaidiwa na Mwinjilisti John Haule.

4. Huduma za Kiroho
Kanisa linatoa huduma mbalimbali za kiroho kanisani na nje ya kanisani inapobidi. Huduma hizo ni kama ifuatavyo:
(a) Ubatizo
(b) Kipaimara
(c) Ibada za shukrani
(d) Misa za Mazishi
(e) Ibada za ndoa
(f) Mikesha mbalimbali
(g) Misa za kumbukumbu
(h) Fellowship
(i) Maombi na Maombezi n.k

5. Vikundi
Kanisa lina vikundi viwili ambavyo ni:-
(a) Umoja wa akina mama (UMAKI).Hukutana kila Alhamisi kuanzia saa 8.00 mchana
(b) Umoja wa Vijana (TAYO). Hukutana kila Jumapili kuanzia saa 10.00 jioni

6. Jumuiya
Tunazo Jumuiya nane zilizotokana na Jumiya tatu za awali. Jumuiya hizi zimeongezeka kwa sababu ya waumini kuendelea kuhamia Majohe, pia kuwasogeza watu kuwa karibu zaidi na kubwa kuliko yote ni kufanya uinjilisti nyumba kwa nyumba kwa kufanya ibada siku za Jumamosi kwenye maeneo yao. Jumuiya hizo ni kama ifuatavyo
(a) Mt. Mariam
(b) Mt. Luka
(c) Mt. Yakobo
(d) Mt. Joseph
(e) Mt. Cecylia
(f) Mt. Yohana
(g) Mt. Marko
(h) Mt. Theresa

7. Kamati
Kanisa lina kamati mbalimbali kama ifuatavyo:
(a) Kamati Tendaji
(b) Kamati ya Uinjilisti Elimu na Ibada
(c) Kamati ya Ujenzi
(d) Kamati ya Maadili na Maadili
(e) Kamati ya Ndoa na Usuluhishi
(f) Kamati ya Mapambo na Mazingira
(g) Kamati ya Ulinzi na Usalama

8. Kwaya na Waimbaji Binafsi
Tunazo kwaya mbili ambazo ni Kwaya ya Uinjilisti na Kwaya ya Sayuni. Pia wapo waimbaji binafsi ambao ni Immanuel Lazaro, Christina Mwaimise, Neema Chimanga na Haleluya Brothers.

9. Sikukuu ya Mt. Mathayo
Kila mwaka mwezi Oktona Kanisa huazimisha sikukuu ya Mtaa ambayo ni Mt. Mathayo na lengo kuu la maadhimisho hayo ni kukusafanya fedha kutoka kwa waumini kwa ajili ya shughuliza ujenzi za hapa kanisani. Kutoka na lengo hilo kila jumuiya hutakiwa kuleta kiasi cha shilingi milioni (2,000.000) na washindi hupewa zawadi mbalimbali.

10. Mipango ya Baadae
Kanisa lipo kwenye mchakato wa kuanzisha ujenzi wa kanisa kubwa na la kisasa na kamati ya ujenzi inaendele na uandaaji wa ramani pamoja na gharama za ujenzi wa kanisa hilo.