Pages

AAAAAAAAAAAA

AAAAAAAAAAAAA

Historia ya Kigango cha Viwege

Muonekano wa Kanisa Anglikana kigango cha VIWEGE

Bwana Yesu Asifiwe.
Awali ya yote tuna tanguliza shukrani za dhati kwa mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kuwa hai hadi hii leo, kwani tuna amini kazi hii ya kupata kigango haikuwa nyepesi ni kwa neema ya Mungu peke yake.

Kigango cha Viwege kimeanzishwa na Mtaa wa Mt. Mathayo na kilifunguliwa mnamo tarehe 14 Desemba, 2015 na Kasisi wa Mtaa Fr. Rev. Patrick Challo. Wakati huo kigango kilikuwa na waumini wa wachache lakini baada ya uinjilishaji mzuri chini ya uongozi makini wa mwinjilisti Sospeter Mrope kwa kushirikiana na waumini wote wa kigango, mpaka sasa tumeweza kuvuna kondoo wa Mungu yaani waumini kama ifuatavyo:

Wanaume 28 Wanawake 30 Watoto 40 Jumla 98

Kwa kipindi hicho kifupi tumeweza kununua eneo la ujenzi wa Kanisa kwa hati ya kisheria, kwa gharama ya T.sh 10,000,000 na hatudaiwi na mwenye eneo.

Kwa jitihada za waumini wote wa kigango cha Viwege, Jumuiya ya Mt. Mariamu na waumini wote wa Mt. Mathayo, tumeweza  kuanzisha ujenzi wa kanisa la muda ambao mpaka sasa unaendelea japo tumekwisha hamia rasmi kwa ibada maalumu iliyozinduliwa tarehe 19 Julai, 2015 na Kasisi wa Mtaa Fr. Rev. Patrick Challo.
 
Pia tumefanikiwa kujenga choo kimoja chenye matundu 2, pamoja na vestori ambayo imefikia usawa wa renta.

Kigango kimefanikiwa kuunda Jumuiya mbili ambazo ni Jumuiya ya Mt. Tito na Mt. Petro ambazo zinafanya ibada zake siku za Jumamosi asubuhi

Asanteni na Mungu Awabariki sana

Karibuni Viwege kwa huduma za kiroho kama ifuatavyo:

SikuTukioMuda
JumapiliIbada1:00 Asubuhi - 3:30 Asubuhi
JumanneKwaya10:00 Jioni -12:00 Jioni
JumatanoFellowship, Maombi na Maombezi09:00 Alasiri -12:00 Jioni
AlhamisiKwaya10:00 Jioni -12:00 Jioni
IjumaaUMAKI10:00 Jioni - 12:00 Jioni
JumamosiMaombi na Maombezi
Kwaya
04:00 Asubuhi - 10:00 Jioni
10:00 Jioni - 12:00 Jioni