Pages

AAAAAAAAAAAA

AAAAAAAAAAAAA

TAYO

Uongozi wa TAYO Achidikonari ya Ilala

Uongozi wa TAYO Mt. Mathayo-Majohe

Historia ya Tayo-Majohe
Kirefu cha neno TAYO ni Tanzania Anglican Youth Organization. Ni umoja wa vijana wa kanisa la Anglikana Tanzania. Katika kanisa la Mt. Mathayo Majohe, umoja huu wa vijana ulianza mwaka 2010, chini ya uongozi wa Marehemu Josiah Malugu ambaye alikuwa mwenyekiti wake, Katibu alikuwa Frank Mgongo na ambapo kwa kipindi hicho kulikuwa na vijana 35. Kila jumapili jioni vijana wa TAYO walikuwa na vipindi tofautitofauti, kama vile michezo na maigizo. Pia kulikuwa na miradi mbalimbali iliyokuwa ikiendeshwa ambayo ni pamoja na uuzaji wa vitabu vya sala, tenzi za rohoni, vitabu vya nyimbo na biblia.

Uongozi wa TAYO ulikuwa kama ifuatavyo:-

Kamati tendaji
Mwenyekiti - Marehemu Josiah Malugu
Mwenyekiti msaidizi - Adella John Bukato
Katibu - Lucas Raphael
Katibu msaidizi - Chance Kamanga
Mhazini - John Mwimbe
Mhazini msaidizi - Beatrice George

Mwaka 2013 ulifanyika uchaguzi wa kupata uongozi mwingine wa TAYO ambapo walikuwa ni kama ifuatavyo:-

Kamati ya tendaji
Mwenyekiti - John Mwimbe
Mwenyekiti msaidizi - Ndaison Jacob
Katibu - Catherine Simon
Katibu msaidizi - Robison Msanga
Mhazini - Agnes John
Mhazini msaidizi - Diana Venance

Tarehe 09/03/2014 kulifanyika uchaguzi mdogo wa kumchagua katibu msaidizi ambaye alikuwa ni ndugu Jonathan Basinda, kutokana na mabadiliko ya mwenyekiti wa TAYO kuteuliwa kuwa katibu wa kanisa kulipelekea kufanyika uchaguzi wa viongozi uliofanyika tarehe 15/03/2015. Hivyo basi viongozi waliopokatikana  ni kama ifuatavyo:-

Kamati tendaji
Mwenyekiti - Ndaison Jacob
Mwenyekiti msaidizi - Veronica James
Katibu - Catherine Simon
Katibu msaidizi - Jonathan Basinda
Mhazini - Diana Venance
Mhazinimsaidizi - Victoria Chane

Kamati tendaji ya sasa
Mwenyekiti   -  John Mwimbe
Mwenyekiti msaidizi -  Lucas Raphael
Katibu    -  Catherine Simon
Katibu msaidizi  -  Ndaison Jacob
Mhazini   -  Veronica James
Mhazini msaidizi  - Elikana Kipala

Mafanikio
1. Ongezeko la idadi ya vijana hasa katika ushiriki wa mambo mbalimbali ikiwemo msiba, vipindi vya ibada, na michezo.

2. Kuandaa semina mbalimbali za ndani na semina ya pamoja ya vijana ambazo zilifundishwa na walimu tofautitofauti kama vile mama Dk. Hiza, Mwinjilisti Sparam Cuthbert Mwambe kutoka Mlandizi n.k.

3. Kufanyika kwa semina ya vijana ya ndani ambayo iliandaliwa na mratibu wa TAYO dayosisi ya Dar es salaam iliyofanyika hapa kanisani ambapo wanenaji walikuwa ni wageni kutoka Texas Marekani.

4. Tumefanikiwa kushiriki kongamano la vijana lililofanyika Bagamoyo kwa kipindi cha siku tatu

5. Tumefanikiwa kushiriki tamasha la vijana la archidikonari ya Ilala katika kanisa la Mt. Mathayo Majohe 08/08/2015, Mt. Thomas Yombo na Mt. Paulo Ukonga ambapo vijana walijitokeza kwa wingi na kuhudhuriwa na kwaya mbalimbali ikiwemo kwaya ya Sayuni na kwaya ya Uinjilisti za hapa kanisani.

6. Kuanzisha miradi mbalimbali kama vile uuzaji wa vitabu na vinywaji.

7. Kuandaa vipindi mbalimbali vya jioni ikama vile kujifunza neno la Mungu, maombi na michezo.

Malengo
i. Kuandaa semina ya mabinti na ya vijana wa kiume peke yao hapa kanisani ikihusisha wazazi wa kiume na wa kike huku wakishirikiana na wanenaji watakaokuwepo kwenye semina hiyo.

ii. Kuwepo kwa miradi itakayoingiza mapato na kukuza ubunifu ndani ya TAYO.

iii. Kuandaa TAYO Familiy Day.